Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amepokea msaada wa madawati 500 yenye thamani ya sh milioni 40 ambayo yalitolewa na Balozi wa China nchini Dk. Lu kwa kushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Goodwill Tanzania Ceramic Bw. Yang.

Balozi Dk.Lu Youqing amemkabidhi msaada huo wa Madawaka wakati Waziri Mkuu Majaliwa alipokuwa akikagua kiwanda cha Vigae(Tales) cha Goodwill Tanzania Ceramic.

Pia Balozi Lu ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuchagua sekta ya viwanda kuwa ndiyo kipaumbele chake katika kukuza uchumi.

Alisema mbali ya ujenzi wa kiwanda cha vigae pia wawekezaji hao kutoka nchini China wanatarajia kujenga viwanda vya mbolea, karatasi na glasi (bilauli).

Tanzania Yachupa Kwa Nafasi 13 Duniani
Sasa Ni Rasmi: Wales Yaipiku England Viwango Vya Soka Duniani