Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry amemfukuza kazi Mwendesha Mashtaka aliyetaka kumfungulia mashtaka kama mshukiwa wa mauaji ya Rais Jovenel Moise baada ya kugundulika kwamba Ariel aliongea kwa simu kwa dakika 7 na mpanga mauaji ya rais huyo.
Hayo yanajiri baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa hivi karibuni waziri mkuu Henry aliitwa mbele ya waendesha mashtaka kutoa maelezo juu ya mawasiliano ya simu aliyoyafanya na moja ya washukiwa wa mauaji ya rais Moise usiku wa siku ya shambulizi.
Taarifa hizo ni kulingana na barua iliyotumwa na ofisi ya mwendesha mashtaka kwenda kwa jaji anayehusika na kesi ya mauaji ya rais Moise ambayo imeorodhesha madai ya kuhusika kwa waziri mkuu Henry kwenye mkasa huo.
Imeelezwa kwamba, Claude alieleza kuwa ushahidi unaonesha anamshuku Henry kwa kumpigia simu Badio, mawasiliano ambayo walifanya Julai 7, 2021 kati ya saa 4:20 asubuhi na ndiyo siku ambayo Rais Moise aliuawa nyumbani kwake na kundi la watu waliovamia makazi yake wakiwa wamejihami kwa silaha na kumshambulia yeye na mkewe kabla ya kumuaa.
“Kuwa na uhakika, hakuna uharibifu, hakuna wito au mwaliko, hakuna ujanja, hakuna vitisho, hakuna kupambana na walinzi waliokuwepo, itanivuruga kutoka katika mipango yangu” Henry amelieleza Shirika la Habari la AP.
Zaidi ya watu 40 wamemekamatwa mpaka sasa kwa kuhusishwa na mauaji ya Rais Moise wakiwemo raia wa haiti na Wanajeshi wa Colombia ambapo bado wanaendelea kumtafuta Badio mshukiwa mkuu na watuhumiwa wengine.