Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 14, 2021 ameshiriki swala ya Eid el Fitr, iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika Swala hiyo Waziri Mkuu amewasihi waumini wa Dini ya kiislam kuhudhuria katika Baraza la Eid litalofanyika katika viwanja vya Kareemjee jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi.

“Niwasihi waislam wenzangu wote, tuhudhurie kwenye Baraza la Eid, mnatambua Rais wetu anakuja kwenye Baraza la Eid kwa mara kwanza ni vyema tukajitokeza kwa wingi kuja kupata neno kwa kiongozi wetu wa nchi,” amesema Majaliwa.

Swala hiyo iliongozwa na Kadhi Mkuu, Sheikh Ali Muhiddini Mkoyogole.

Tusherehekee kwa kiasi - RC Kunenge
DPP awafutia mashtaka vigogo, waachiwa huru