Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika halmashauri mbili za wilaya ya Kilombero kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya sh. bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi ha oleo Septemba 15, 2019 wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Sambamba na kuwasimamisha kazi watumishi hao, ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Watumishi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.

Majaliwa amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda.

Amesema katika mitambo kumi ya ukusanyaji wa mapato iliokaguliwa imeonyesha kiasi cha shilingi milioni 348 zilizokusanywa hazikupelekwa bank na hivyo kuishia mikononi mwa watu.

Katika uchunguzi huo ilibainika kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti mbalimbali za watumishi wa halamshauri hizo kutoka kwa mtendaji wa Kata ya Viwanja 60 katika Mji wa Ifakara aitwaye Gregory Midas.

Watumishi hao ni Reina Mrema ambaye anadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 298, Haile Njitango milioni 73 , Linus Mdembo kiasi cha shilingi milioni 2 kwa kushirikiana na mtendaji huyo wa Kata.

Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika halmashauri ya Mji wa Ifakara, John Mvanga ambaye ndiye alibaini kuwepo na ubadhilifu wa fedha hizo na badaye kusimamishwa kazi, arejeshwe kazini mara moja na asibugudhiwe.

Teknolojia 10 zilizovumbuliwa na wanawake
Norwich yaivuruga Man City, yaweka historia