Waziri Kassim Majaliwa amezungumza na wakazi wa mkoa wa Dodoma leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. 

Kati ya mambo aliyozungumzia Waziri Majaliwa ni uwamuzi wake wa kuhamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi.

“Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” Majaliwa

Amesema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja

 

Waziri Mkuu amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

 Wakazi wa Dodoma wametakiwa kutumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.

Pia Rais wa Tanzania, John Pombe Magudfuli akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma kwenye uwanja wa mashujaa huku akishangiliwa amesema atahakikisha Dodoma inakuwa makao makuu ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobakia kwenye awamu ya kwnza ya uongozi wake ili kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma..

 

Magufuli – “Kama wabunge karibu 300 na mawaziri na manaibu wao ambao hawafiki 30 wanakaa hapa kwa miezi mitatu na maisha yanakwenda, kama makao makuu ya chama kinachotawala nchi yako hapa sioni sababu ni kwa nini Serikali ninayoiongoza iendelee kubakia Dar es Salaam,” 

 

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza Jumamosi iliyopita, Julai 23, 2016 wakati akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho.

 Rais  amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi mashujaa walioipigania nchi hii, pia amewasisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani iliyokuwepo nchini.

Picha: Matukio 4 ya Mwisho wa Wiki
Hull City Yadhaminiwa Na Kampuni Ya Kenya