Waziri Mkuu wa Sudan aliyeondolewa madarakani Abdalla Hamdok anatarajiwa kurejeshwa madarakani, baada ya kuwekwa katika kifungo cha nyumbani wakati wa mapinduzi ya ghafla ya kijeshi mwezi uliopita.
Wafungwa wote wa kisiasa wataachiliwa kama sehemu ya makubaliano mapya kati ya wanajeshi, viongozi wa kiraia na makundi ya waasi wa zamani, wapatanishi wamesema.
Tarehe 25 Oktoba, jenerali wa kijeshi wa Sudan ghafla alitangaza hali ya hatari na kuvunja uongozi wa kiraia, Hamdok amekubali masharti ya kukomesha umwagaji damu zaidi, shirika la habari la Reuters linaripoti, likinukuu chanzo kilicho karibu naye.