Lydia Mollel – Morogoro.
Wananchi wa Kata ya Mindu iliyopo Mkoani Morogoro, wamemuomba Mbunge wa Morogoro mjini, Aziz Abood, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na kufika katika eneo hilo na kusikiliza na kutatua kero inayiowakabili juu ya fidia ya kupisha eneo la Bwawa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Dar24 Media, Wananchi hao wamesema hawana nia ya kukaidi agizo la Serikali la kupisha eneo hilo, bali wanalalamikia fidia waliyotangaziwa kulipwa ambayo ni ndogo ikilinganishwa na gharama za ujenzi zilivyo kwasasa.
Akizungumzia sakata hilo, Diwani wa Kata ya Mindu, Zuberi Mkalaboko ameiomba Serikali kusikiliza malalamiko ya wananchi hao, kwani Baraza la Mawaziri lilipotoshwa na Mamlaka kwa namna wanavyoendesha zoezi hilo na utaratibu wa ulipaji fidia katika maamuzi yaliyofanyika.
Hata hivyo, hatua ya wananchi hao, inakuja ikiwa ni siku kadhaa tangu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa kuwatembelea NA kutoa maelekezo ya kuwalipa fidia Wananchi waliopo ndani ya mita 500 za Bwawa la Mindu, ili wapishe eneo hilo.