Serikali nchini, imeendelea kuboresha hali ya masoko ya samaki nchini kupitia ujenzi wa masoko mbalimbali ya samaki, huku ikisema itaendelea kuimarisha Shirika la Uvuvi Tanzania, usimamizi na udhibiti wa ubora, usalama na viwango vya samaki na mazao ya uvuvi pamoja na kuimarisha huduma za utafiti, mafunzo na ugani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameyasema hayo jijini Dodoma nakuongeza kuwa pia Serikali itaimarisha miundombinu ya masoko ya samaki, vituo vya kuendeleza ukuzaji wa viumbe maji na kuanza ujenzi wa meli za uvuvi katika bahari kuu.

Ameyataja masoko yaliyoboreshwa kuwa ni Zingibari (Halmashauri ya Mkinga), Kipumbwi (Pangani), Ng’ombo (Nyasa), Manda (Ludewa), Maporomoko (Tunduma), Kyamkwikwi (Muleba), Nyamikoma (Busega) pamoja na mialo ya kupokelea samaki katika Halmashauri za Momba (Masuche), Nkasi (Karungu) na Chato (Chato beach).

“Katika mwaka 2023/2024, Serikali itaendelea kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora za mifugo, malisho, vyakula vya mifugo na maji. Vilevile, itatoa kipaumbele katika kuimarisha afya ya mifugo, kuboresha huduma za ugani, kuanzisha na kuendeleza vituo atamizi vya uwekezaji vya vijana, kuimarisha
huduma za utafiti na mafunzo ya taaluma za mifugo.” amesema Waziri Mkuu.

Mtwara: Hakimu kizimbani kwa rushwa ya 50,000
Meridianbet yaja na Sloti yenye Ushindi Rahisi