Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amejiuzulu ili kuweza kusaidia kutatua mgogoro wa kisiasa ulioigubika nchi hiyo.
Kiongozi huyo amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa chama chake cha Ethiopia People’s Demecratic front, ambapo mpaka sasa haijabainika iwapo chama hicho kimekubali uamuzi wake wa kujiuzulu.
“Ili kupata suluhu na ufanisi wa mabadiliko yaliowekwa, na suluhu tuliyoiweka nimewasilisha barua ya kujizulu majukumu yangu katika serikali na katika chama kwa hiari yangu, amesema katika hotuba iliyorushwa hewani moja kwa moja na Televisheni ya taifa ya EBCTV.
Hata hivyo, nchi hiyo imeingia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa ambao umesabaibisha vifo vya watu kadhaa na wengine kshikiliwa na polisi katika magereza mbalimbali nchini humo.