Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Hamed Bakayoko amefariki dunia katika hospitali iliyoko nchini Ujerumani, alipokwenda kupatiwa Matibabu ya Saratani.

Bakayoko ambayo ana miaka 56 aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mwezi Julai mwaka 2020 baada ya mtangulizi wake Amadou Gon Coulibaly kufariki.

Alipelekwa Ufaransa  mwezi Februari kwaajili ya matibabu na alihamishwa Ujerumani kwa sababu afya yake iliendelea kuzorota.

Bakayoko amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vyombo vya Habari na alitekeleza jukumu kubwa katika maridhiano nchini Ivory Coast wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1993.

Viongozi waonya uzushi unaoendelea mitandaoni
Serikali kuanzisha vituo vya uhakiki wa bidhaa