Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) Firmin Ngrebada, amewasilisha ombi la kujiuzulu kwake kwa Rais Faustin Archange Touadera.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika ujumbe kuwa, Ngrebada aliripoti kwamba yeye na baraza lake la mawaziri waliwasilisha ombi la kujiuzulu kwao kwa Rais Touadera.

Ngrebada amekuwa akihudumu kama waziri mkuu wa serikali tangu mwaka 2019.

Hata hivyo Rais Touadera anatarajiwa kutangaza baraza jipya la mawaziri hivi karibuni.

Wakala wa Bwalya aichimba mkwara Simba SC
Aliyempiga kofi Rais Macron ahukumiwa kifungo cha miezi minne