Kiongozi mkuu wa kiraia na Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok amezuiliwa na wanajeshi pamoja na mawaziri wengine kadhaa katika nyumba yake.

Mapinduzi yanayoendelea nchini Sudan ni mzozo wa hivi karibuni katika kipindi cha machafuko kwa nchi hiyo katika matokeo ya kutoaminiana kati ya viongozi wa kijeshi na raia.

Ingawa vikundi hivyo viwili vimekuwa vikipingana hadharani bado nchi hiyo inatakiwa kuwa katika mpito wa raia na viongozi wa jeshi kuendesha nchi pamoja kwenye kamati ya pamoja inayojulikana kama Baraza Kuu.

Mtandao, vituo vya radio na usafiri wa watu kutoka sehemu moja hadi nyingine na maeneo yote yanayoweza kutoa habari kwa haraka pia yamezuiliwa ikiwa Picha na ripoti zingine zinazotoka katika mji mkuu, Khartoum, zinaonyesha kwamba kuna waandamanaji nje ya jiji.

Waandamanaji wanaounga mkono jeshi wameishutumu serikali kwa kushindwa kufufua utajiri wa nchi hiyo wakati uhaba wa mkate ukizidi ikiwa hatua za Hamdok za kurekebisha uchumi pamoja na kupunguza ruzuku ya mafuta hazijapendwa na wengine.

Wanajeshi na Raia nchini Sudan wamekuwa wakigawana madaraka tangu Agosti 2019 kufuatia kupinduliwa kwa Rais Omar al-Bashir aliyehudumu kwa muda mrefu mapema mwaka huo.

Omar Al Bashir alipinduliwa na wanajeshi lakini maandamano ya kila mara yalilazimisha wanajeshi kujadili mpango uliolenga kuhamia serikali ya kidemokrasia.

Unamtafsiri vipi Kanye "YE"?
Vijana wapongezwa kwa uwekezaji