Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson leo ameitisha mkutano wa dharura, wakati ambapo nchi kadhaa zinaendelea kuzizuia ndege zao kwenda Uingereza ili kuzuia kuenea kwa aina mpya ya virusi vya corona vilivyogunduliwa nchini humo. 

Johnson ameitisha mkutano wa kamati ya dharura ya mawaziri kujadili marufuku ya safari za ndege za abiria za kimataifa. 

Nchi nyingi za Ulaya tayari zimezuia ndege na wasafiri kutoka Uingereza, huku nchi zaidi zikitarajiwa kuchukua uamuzi kama huo.

Shirika la Afya Duniani, WHO pia limetoa wito wa hatua kali kuchukuliwa Ulaya, ambako hadi sasa zaidi ya watu 500,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Mkuu wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel jana walizungumza kwa njia ya simu kuhusu suala hilo.

Wivu wa mapenzi chanzo cha mauaji mengi nchini
Jafo awataka wakurugenzi kutoa maelezo juu ya hili