Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ameomba radhi kwa viongozi wa nchi za Caribbean baada ya serikali yake kutishia kuwafukuza Uingereza watu waliohamia nchini humo miaka ya 1950 na 1960.

Ameyasema hayo katika mkutano uliofanyika Downing Street nchini Uingereza, ambapo amewaambia wawakilishi wa nchi 12 za Caribbean wanachama wa Jumuiya ya madola kuwa amelizingatia suala la wahamiaji hao kwa umakini mkubwa.

“Nataka niwatoe hofu ya kwamba serikali yangu haina mpango wa kuwafukuza wananchi wa Jumuiya ya Madola, hasa wale wa nchi za Caribbean waliokuja kutafuta maisha na kuishi hapa, suala hili la wahamiaji nalichukulia kwa umakini mkubwa sana, naombeni radhi kwa kuwasababishia wasiwasi na hofu.”amesema May

Aidha, Serikali ya Uingereza imekosolewa vikali kwa jinsi ilivyowashughulikia watu waliyohamia nchini Uingereza kati ya mwaka 1948 wakati meli ya Windrush ilipowasili na kundi la kwanza la wahamiaji wa Caribbean mapema miaka ya 1970 waliotokea eneo linalojulikana kama West Indies, makoloni ya zamani ya Uingereza katika Carribean.

Hata hivyo, Wahamiaji hao na wazazi wao walialikwa nchini Uingereza kwa lengo la kusaidia kuijenga upya nchi hiyo baada ya vita kuu ya pili vya dunia, wakati wengi wao kihalali walikuwa Waingereza baada ya kuzaliwa nchi yao ikiwa iko chini ya koloni la Uingereza na wakapewa nafasi ya kubakia huko milele.

 

 

 

Video: Polisi yashikilia paspoti ya Diamond, Prof. Ndalichako awasha moto bungeni
Mke wa rais wa zamani wa Marekani afariki dunia