Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amepimwa na kuthibitika kuwa na virusi vya Corona leo huku akitangaza kuendelea kuwa mkuu wa shughuli za kukabiliana na mzozo wa virusi hivyo.
kulinga na taarifa iliyotolewa na ofisi yake yake maarufu No 10, waziri Mkuu huyo wa amesema kuwa ataendelea kuliongoza taifa kutoka nyumbani baada ya kupatikana na Covid-19.
“Nimekuwa na dalili ndogo za coronavirus, ambazo ni viwango vya juu vya joto la mwili na kikohozi ambacho hakikomi ,” amesema Johnson katika video aliyoituma kwenye ukurasa wake Twitter.
”Ninaweza kuendelea, nashukuru teknolojia kwamba ninaweza kuwasiliana na viongozi wakuu na kuongoza taifa dhidi ya virus.”, amesisitiza.
Hata hivyo waziri mkuu huyo atajitenga binafsi katika makao yake ya kikazi ya Downing Street,na muhudumu wa huduma za afya nchini Uingereza.
Ikumbukwe kuwa Mwanamfalme Charles wa Wales amekutwa na virus hivyo mapema wiki hii.
Kuna visa zaidi ya 11,600 vilivyothibitishwa vya coronavirus nchini Uingereza , na watu 578 wamepoteza maisha.