Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesikitishwa na Viongozi wa Chama Cha Soka mkoani Mbeya, Klabu ya Mbeya City na wasimamizi wa uwanja wa CCM Sokoine kwa kuruhusu mashabiki wengi kuingia uwanjani na kukaa bila kufuata mwongozo wa Wizara ya Afya kuhusu kujikinga na Ugonjwa wa Corona.
Waziri Mwakyembe ametoa onyo Kali kwa Klabu ya Mbeya City, Viongozi wa Chama Cha Soka mkoa wa Mbeya na wasimamizi wa uwanja huo kuacha Mara moja kuruhusu Mashabiki kujaa uwanjani na kukiuka taratibu za Serikali na amewaomba tukio hilo lisijitokeze tena kwenye mchezo ujao wa ligi kuu Tanzania Bara Jumapili Kati ya TZ Prisons na Simba.
Kwenye mchezo huo mashabiki walijitokeza kwa wingi huku wakisahau kufuata muongozo uliotolewa na Serikali kwa kukaa umbali wa mita moja ili kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona.
Timu ya kwanza ambayo ilikutana na rugu la Serikali ni JKT Tanzania ambayo ilifanya hivyo Juni 17 ilipomenyana na Yanga kwenye sare ya kufungana bao 1-1.
Lengo kubwa ambalo linafanywa na Serikali ni kulinda afya za mashabiki na watanzania kiujumla.