Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro ameipongeza timu ya taifa ya mchezo wa kuogelea (The Tanzanite) kwa kuibuka washindi wa pili wa jumla katika mashindano ya The 8 African Zone II Championship yaliyofanyika kuanzia Novemba 23 hadi 25 Kigali, Rwanda.

Katika mashindano hayo Tanzania mbali na kumaliza nafasi ya pili lakini pia walifanikiwa kubeba makombe manne pamoja na medali 87 ikiweno dhahabu 4, fedha 43 na shaba 40.

Kwa mujibu wa taarita iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo jana, Dk Ndumbaro alisema ushindi wa timu hiyo umeliletea heshima taifa na kuitangaza vyema Tanzania kimataifa kupitia tasnia ya michezo ambayo ni ishara ya kukua kwa mchezo wa kuogelea hapa nchini.

“Nawapongeza viongozi pamoja na wachezaji wote kwa kujituma na kupambana kwa ari kubwa na kuibuka na ushindi, hii ni ishara kuwa mchezo wakuogelea unaendelea kukua kwa kasi na kufanya vizuri kweye mashindano mbalimbali ya kimataifa,” alisema Ndumbaro.

Katika mashindano hayo timu ya Tanzania ilishiriki ikiwa na jumla ya viongozi 10 na wachezaji 30 na kuibuka mshindi wa pili wa jumla kati ya mataila 10 yaliyoshiriki mashindano hayo ikiwemo Uganda, Tanzania, Kenya, Burundi, Afrika Kusini, Eswatini, Eritrea, Dibouti, Ethiopia na wenyeji Rwanda.

Chama: Tuna mzuka wa kupambana
UKIMWI: Maambukizi mapya kwa Watu wazima yapungua