Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amekutana na Watumishi wa Idara ya kinga na kujadili masuala mbalimbali ya kinga na malengo waliojiwekea ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Idara katika kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wenye uhitaji.
Amezungumza na watumishi hao leo Januari 17, 2022 katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Abel Makubi pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe.
Katika kikao hicho, Waziri Ummy amesisitiza juu ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi ili kupunguza kero na malalamiko katika jamii katika nyanja zote, ikiwemo katika huduma za mama na mtoto na huduma za lishe.