Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ), Ummy Mwalimu ametangaza Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa shule za Serikali na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi mwaka 2021 ambapo amesema idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 14.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 1, 2021 Jijini Dodoma Waziri Ummy amesema ongezeko hilo linatokana na jumla ya watahiniwa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa shule za Serikali na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi mwaka 2021 kufikia 148,127 kutoka 129,854 mwaka 2020.

Aidha, Idadi hiyo ya wanafunzi wenye sifa za kujiunga na udahili huo pia imejumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu 288 wakiwemo wasichana 123 na wavulana 165.

Bonyeza hapa chini kutazama majina ya waliopangiwa kujiunga kidato cha tano 2021

Ameeleza kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa kuzingatia takwimu za wanafunzi waliofanya mtihani mwaka 2020 kutoka Tanzania Bara ambapo watahiniwa waliopata daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 153,464 ikiwa ni wasichana 67,135 na wavulana 86,329, sawa na asilimia 35.06 ya watahiniwa wote.

Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea waliomaliza kidato cha nne mwaka 2020 wakiwa chini ya Taasisi ya Elimu ya watu wazima ambao walipata daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 479 ikiwa wasichana ni 289 na wavulana 190.

Sey amvulia kofia Morrison
Polisi Tanzania waitishia Simba SC