Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu, amewataka wakuu wa shule wasiwazuie wanafunzi kuanza masomo pale wanapokuwa hawana sare za shule, bali watoe muda kwa wazazi walau wa mwezi mmoja ili waweze kuwanunulia watoto wao sare.

Waziri Ummy amesema lengo la kutoa agizo hilo ni kuhakikisha wanaondoa vikwazo vinavyoweza kupelekea mtoto kushindwa kuanza masomo yake kwa wakati.

“Nimesema kama January 17 imefika mwanafunzi hana sare za shule aruhusiwe kuingia darasani, mpe mzazi wiki 2 au mwezi, sijasema kwamba mtoto asiingie na uniform mwaka mzima, tunachotaka ni kuondoa vikwazo visivyo vya lazima kwa watoto wetu kupata elimu,” amesema Waziri Ummy.

Rais Samia ashiriki mkutano wa EAC kwa njia ya mtandao
Simba yapokewa kwa shangwe Tabora