Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ummy Mwalimu, amesema Serikali itajenga barabara ya Lami yenye urefu wa KM 13 ya Nzughuni- Mahomanyika Jijini Dodoma ili kuboresha mazingira ya Kata hiyo ambayo wananchi wamekua wakipata changamoto sana wakati wa mvua.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo Septemba 3, 2021 wakati wa ziara yake Jijini Dodoma ya kukagua ujenzi wa barabara za Mwangaza-Kisasa-Medeli, Nzughuni-Mahomanyika na ujenzi wa mifereji ya Mlimwa.
“Nzughuni kuna idadi kubwa ya watu na eneo hili wakati wa Mvua linajaa maji hakupitiki lakini taarifa nlizopewa hapa ni kuwa fedha iliyotengwa ninya kujenga Barabara ya urefu wa KM 1.7 tu sasa nawaagiza TARURA waombe fedha za dharura kwa ajili ya kuweka lami barabara yote ya Nzughuni yenye urefu wa Km 13,” Amesema Waziri Ummy.
“TARURA mnaweza kuanza kujenga Kwa awamu mkaanza na KM 5 kwa mwaka huu wa fedha kisha mkamalizia zingine mwaka unaofuata ila cha Msingo barabara hii yote iwekwe lami ili tuzidi kuboresha muonekano wa Makao Makuu Dodoma,” Ameongeza Waziri Ummy.
Naye Mbunge wa Dodoma Anthony Mavunde amemshkuru Waziri Ummy kwa kuskia kilio cha Wananchi wa Nzughuni na ameomba zaidi kuwa Daraja linalounganisha Nzuguni A na B ambalo limekua likileta maafa wakati wa mvua na changamoto kubwa kwa Wananchi liingizwe kwenye mpango wa ujenzi.
Sambamba na hayo yote Waziri Ummy amehitimisha ziara yake kwa kuwaambia TARURA waangalie namna wanavyoweza kuliingiza daraja hilo kwenye mpango mara ambapo ujenzi wa barabara hiyo ya Nzughuni- Mahomanyika utakapoanza