Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Mtendaji wa kijiji cha Nyamililo Wilayani Sengerema Mariamu Mgunda, pamoja na mwenyekiti wa Kijiji hicho Mateso Shibayi na kuwaweka ndani kwa kosa la kuchangisha kwa nguvu fedha za ujenzi wa jengo la Zahanati.

Waziri Ummy amesema hayo akiwa akiwa katika ziara mkoani humo, baada ya wananchi kulalamikia mambo wanayofanyiwa na viongozi hao ikiwamo kukamata mifugo kwa kushindwa kutoa mchango.

Aidha, ameagiza watendaji wote wa vijiji na kata nchi nzima wasichangishe fedha kwa wananchi bila kibali kutoka kwa mkuu wa wilaya husikia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriey amesema atafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo na atakayebainika atafikishwa Mahakamani.

Naye, Mariamu Mugunda amesema michango hiyo walikubaliana na wananchi kupitia vikao vyote vya kijiji hicho na hajaenda kinyume na utaratibu.

Zingatia haya kabla ya kupata chanjo
Waziri Mkuu: Tumechochea uwekezaji