Waziri wa Nchi, Ofisi a Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa walioapishwa leo kwenda kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri zilizopo ndani ya Mikoa yao.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Juni 21, 2021 wakati akizungumza katika hafla ya uapisho wa Wakuu wa Mikoa ya Tabora na Shinyanga iliyofanyika Ikulu, Mkoani Dodoma ambapo amegusia mwenendo wa upelekaji fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri za Mikoa hiyo.

“Mkoa wa Tabora una changamoto ya ukusanyaji wa Mapato wa mapato ya ndani ya Halmashauri Mhe. Rais ameagiza tukakusanye, Dkt. Batilda Buriani uliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huo ukalisimamie kikamilifu”

“Shinyanga kwenye Ukusanyaji wa mapato ya ndani mmefikia asilimia 74 lakini upelekaji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo bado hamfanyi vizuri. Kahama Manispaa ndio amepeleka 38% na Shinyanga Manispaa amepeleka 14% tu hivyo mkalisimamie na hili”

” Nasisitiza kwa Kila Halmashauri kuwa ukikusanya sh. 100 basi sh. 40 iende kwenye miradi ya maendeleo na miradi hiyo iwe ile inayotatua kero za Wananchi kwenye maeneo ya Afya, Elimu na Miundombinu”

“Mhe Rais Samia nikushukuru sana kwa Kumteua Fatma Mganga kuwa RAS nilipita kwenye Halmashauri yake ya Bahi hakuwa na mapato makubwa Mil 800 tu lakini alipeleka 106% kwenye miradi ya maendeleo zaidi,” amesema Waziri Yum.

Mbunge alia na Bureau De Change
Young Africans yaachwa kwenye mataa