Waziri wa Elimu nchini Kenya, Amina Mohammed amejikuta katika kashfa ya rushwa inayohusisha kompyuta ambazo Rais Uhuru Kenyatta alinunua kwa lengo la kuzisambaza katika shule mbalimbali za za sekondari zilizo chini ya Serikali.
Kulingana na ripoti ya ukaguzi ya jenerali, Edward Ouko, Wizara hiyo imeshindwa kupata hesabu zaidi ya kompyuta 2000 ambazo hazionekani na zilitakiwa kuwa tayari zimekwisha pelekwa katika shule husika za sekondari.
Pia ripoti hiyo ya ukaguzi imeonesha kuwa Wizara iliyoongozwa na Amina Mohammed ilinunua kompyuta 3,320 kwa shule za sekondari lakini iliweza kutoa kompyuta 1,107 tu.
Mkaguzi amesema kuwa kompyuta zilizopotea zilikuwa na thamani ya shilingi milioni 153 za Kikenya sawa na bilioni 343 za Kitanzania ambapo ni sawa na kompyuta 2,213 ambazo hazionekani.
Wizara hiyo pia ilionekana kuwa imetumia shillingi milioni 1 za Kikenya kwa safari licha ya ugawaji wa Shilingi 440, 000 za Kikenya.