Waziri Mkuu wa Libya, amemsimamisha kazi Waziri wa mambo ya kigeni, Najla Mangoush na kuamuru achunguzwe baada ya Israel kusema kwamba alikutana na waziri wake wa mambo ya kigeni Eli Cohen wiki iliyopita, licha ya mataifa yao kutokuwa na uhusiano rasmi wa kidiplomasia.
Tukio hilo linakuja baada ya Cohen akydai kwamba walizungumza na Mangoush kuhusu umuhimu wa kudumisha turathi za kiyahudi nchini Libya, taarifa ya Israel kuhusu mkutano huo uliofanyikia Italy zilipelekea maandamano madogo nchini Libya, ambayo haitambui Israel.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Libya, Najla Mangoush
Wizara ya mambo ya kigeni ya Libya, imesema Mangoush alikuwa amekataa kufanya mkutano na wawakilishi wa Israel, na kwamba kilichpofanyika ni kwamba walikutana nao bila kukusudia kwenye ofisi za wizara ya mambo ya kigeni ya Italy.
Tangu 2020, Israel imejitahidi kurejesha ushusiano wake na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, Bahrain, Morocco na Sudan, kupitia mkataba maarufu kama Abraham accords, iliosimamiwa na Marekani.