Mkuu wa zamani wa Jeshi la Uganda na Waziri wa sasa wa Ujenzi na Uchukuzi, Jenerali Katumba Wamala amepigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana karibu na nyumba yake katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala.

Hata hivyo Jenerali Katumba ambae amejuruhiwa kwenye mkono amempoteza binti yake na dereva wake papo hapo katika tukio hilo.

Aidha walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa watu hao wenye silaha na kumimina risasi kwenye gari la Jenerali Wamala walikuwa kwenye pikipiki.

Kwa miaka michache iliyopita, nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na mashambulizi kama hayo ya watu wenye silaha wanaoendesha pikipiki.

Jenerali Wamala alikuwa mkuu wa jeshi la UPDF mwaka 2013 hadi 2017, baadaye akapewa cheo cha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na sasa ni mmoja wa Wabunge 10 wanaowakilisha jeshi la UPDF katika Bunge la 11.

Mwaka 2001 hadi 2005 alikuwa Mkuu wa Jeshi la polisi (IGP).

Waziri Mkuu aagiza matumizi ya nishati mbadala
Jaji Mtanzania achaguliwa kuongoza Mahakama ya Afrika