Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mh. Heiko Maas anatarajia kuanza rasmi ziara yake barani Afrika ambapo leo hii ametua nchini Ethiopia na baadaye kuelekea nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili kuanzia kesho tarehe 3 Mei mpaka tarehe 4 Mei mwaka huu.

Waziri huyo ameamua kutembelea Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano uliopo na kuibua maeneo mapya katika ushirikiano huo.

Taarifa hiyo imetolewa leo mbele ya waandishi wa habari na Kaimu Mkurugenzi idara ya Ulaya na Marekani, Jestas Nyamanga

”Waziri atakuja kesho akiwa na ndege binafsi akiambatana na ujumbe wa watu hamsini, ni ziara yake ya kwanza kuja Tanzania na bara la Afrika tangu alipoteuliwa mwezi machi mwaka huu” hayo yamesemwa na Nyamanga.

Aidha mbali na hayo yaliyotajwa hapo juu Waziri Maas anatarajiwa katika ziara hiyo kuweka shada la maua kwenye sanamu la Askari kama kuwakumbuka waliopigana katika vita kuu ya Dunia.

 

 

Kamati ya wakimbizi Rwanda yavunjwa
Aliyekuwa Katibu Mwenezi CCM auawa kwa kupigwa risasi