Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amesema anatarajia kukutana   na wasanii wa makundi yote katika kipindi kifupi kijacho ili kujua   changamoto zinazowakabili kwenye kazi zao ili kupata ufumbuzi wa pamoja.

Ameyasema hayo leo Februari 3, 2022 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Jacqueline Woiso katika ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.

Amefafanua kuwa ili kuleta mapinduzi katika sanaa kuna haja ya Serikali kukaa pamoja na wadau ili kujua changamoto na kuzitatua kwa pamoja.

Nitahakikisha tunakwenda kuwanyanyua na kuboresha kazi za wasanii wetu na kuziweka katika ubora wa kimataifa kwa kushirikiana nao ili wafaidike na kazi zao” Amesema Mchengerwa.

 Aidha, ametoa wito kwa wadau wote ikiwa ni pamoja na Multichoice Tanzania kutoa ushirikiano kwa  Serikali ili kuweza kufanikisha azma ya Serikali  ya kutoa ajira na kuboresha maisha ya wasanii hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo, ameahidi ushirikiano wa karibu na Wizara katika kuhakikisha sanaa inakuwa na wasanii wanapata kipato kutokana na kazi zao.

Mbarawa atoa ufafanuzi daraja la Tanzanite
Mradi wa kuwekeza kwa watu kukamilika