Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, ameiagiza Bodi yaKampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kuwanyang’anya wawekezajiranchi zote walizokodishwa na kushindwa kulipa madeni.

Akitoa maagizo hayo, akiwa wilayani Mbarali mkoani Mbeya wakati akizungumza na wakulima na wafugaji katika Bonde la Usangu, Ndaki amesema serikali inahitaji ranchi zote zilipe madeni kuanzia Januari 12 hadi Februari 15, mwaka huu na kwamba zitakazoshindwa kulipa, zinyang’anywe na kupewa wawekezaji wengine.

Pia alipiga marufuku kufanyika kwa shughuli za kilimo kwenye maeneo ya ranchi kwa madai kuwa ni kwenda kinyumecha makubaliano ya mkataba.

“Nimetoa muda wa kuanzia Januari 12 hadi Februari 15 majira ya saa saba mchana, Bodi ya NARCO iwe imekusanyamadeni yote wanayoyadai kwenye ranchi mbalimbali nchini, lakini pia wawekezaji kufuata makubaliano ya mikataba ilikila upande unufaike na ranchi hizo,” amesema Ndaki.

Katika hatua nyingine, Ndaki aliwahakikishia wawekezaji katika wa ranchi mbalimbali nchini kwamba serikali imewaandalia mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao na kuomba waendelee kushirikiana.

Katibu wa wizara hiyo prof. Gabriel Ole Sante aliwaomba wamiliki wa ranchi kutumia maeneo hayo kwa ajili ya mifugo na shughuli zingine ambazo ni kinyume na makubaliano.

PICHA: AMAVUBI watangulia CHAN
Kocha Ibenge aitamani Simba SC, lakini.....