Rais mteule nchini Liberia, George Weah amewashauri raia wa Liberia wanaoishi nchi za ng’ambo kurudi nyumbani ili kusaidia kuijenga nchi yao.

Nyota wa huyo zamani wa mpira wa miguu ambaye amechaguliwa kuwa Rais, amesema hayo wakati wa mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu atangazwe mshindi katika uchaguzi wa urais nchini humo.

Amesema ujuzi wa watu wa Liberia walio nchi za kigeni unahitajika kuijenga nchi hiyo.

Aidha, Rais Weah amepongezwa baada ya kusema kuwa ufisadi hautavumiliwa katika utawala wake, ambapo Januari 2018 anaingia madarakani rasmi.

Mbowe: Futeni vyama vingi kama havina umuhimu
Coutinho kutimkia Barcelona