Ili kuepusha taharuki zinazotokea katika jamii kutokana na kukosekana kwa usiri unaotokana na matukio ya ukatili kwa Watoto, Taasisi zinazopambana na vitendo vya ukatili zimetakiwa kuajiri wafanyakazi wenye weledi.

Hayo yamebainishwa na Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania – TAWLA, Mwanaidi Kombo ambaye amesema kuajiri wafanyakazi wasio na weledi kumechangia utoaji wa taarifa za waathirika wa vitendo vya ukatili, ambazo zilipaswa kuwa siri.

Amesema, “weledi utaepusha hizi taharuki, lazima tujue tunapeleka watu wa namna gani katika suala zima la utoaji wa elimu, tunapeleka watu wa namna gani katika kuwahudumia hawa waathirika wa ukatili wa kijinsia.” 

Takwimu za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu inaonesha kuwa mwaka 2022 jumla ya watoto 12,163 walifanyiwa ukatili na kati ya hao 6,365 ilikuwa ni matukio ya ubakaji ikilinganishwa na miaka ya 2021/2022 ambapo watoto 5,899 walifanyiwa vitendo vya ubakaji.

Mapigano ya kikabila yauwa 32
Rasilimali za ardhini kuchorewa ramani