Muigizaji wa Bongo Movies, Wema Abraham Sepetu ametoa kilicho ndani ya moyo wake kufuatia tukio  la kusikitisha la kuharibika kwa ujauzito wake wa mapacha jana usiku.

Wema ambaye leo habari yake imeongozwa kwa kuzungumziwa zaidi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa upande wa burudani na kuzua gumzo, ameeleza jinsi alivyoumizwa na tukio hilo huku akimtanguliza Mungu na kuwashukuru mashabiki wake.

“Ni kweli. Na imeniuma sana lakini nimefika kwenye hatua maishani mwangu naweza kusema Alhamdulillah for everything.Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilionao na wameonyesha moyo wa kibinadamu. Nawashukuru kwa upendo wenu, MNANIPA NGUVU.

Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilionao na wamefurahia kwasababu zao binafsi. Nawashukuru kwa uwepo wenu, MNANIPA UJASIRI.

Alhamdulillah kwa siku ya kesho. Ilimradi nina pumzi, SITACHOKA KUJARIBU TENA.

Hata ukikosa, ukakosa, ukokosa eeeeeeh…sema ASANTE, KWELI YEYE NI MUNGU,” Wema ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Waziri Mkuu Afanya Ziara Katika Uwanja Wa Uhuru
Wakurugenzi wa wanne wa halmashauri wafyekwa, wahonga wakaguzi wa CAG kuficha uchafu