Muigizaji wa filamu za Bongo, na Kipenzi cha watanzania Wema Sepetu maarufu kama TZ Sweetheart amesafiri kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ambapo imeelezwa kuwa atafanyiwa upasuaji.
Hayo yameelezwa leo na Mama mzazi wa mlimbwende huyo, Mariam Isaack Sepetu mahakamani pindi mahakama ilipohoji sababu za kutohudhuria kwa mtuhumiwa huyo juu ya kesi yake inayomkabili ya kutumia madawa ya kulevya ambayo ilikuwa isikilizwe leo.
Hata hivyo mama Wema hajaweka wazi tatizo linalomsumbua Wema Sepetu na kupelekea kusafirishwa nchini India kwa upasuaji.
Mama wa Wema amesema kuwa mwanae ameshindwa kuhudhuria kesi hiyo kutokana kuwa hayupo nchini amesafiri kwenda India kufanyiwa matibabu na katika kuthibitisha hilo alitoa baadhi ya nyaraka za kusafiria ili kuiaminisha mahakama ambayo ilianza kutilia shaka taarifa hizo.
-
Mpoto achochea bifu la Alikiba na Diamond
-
Video: Itazame ngoma mpya ya Belle 9
-
Makala: Wimbo wa Mpoto ulihitaji kiki ya uongo ya MC Pilipili na ..?
Aidha kesi hiyo imehairishwa mpaka June 13, 2018 ambapo Hakimu aliyeendesha kesi hiyo hajaridhishwa na vithibitisho vilivyoneshwa kuwa Wema amesafiri na kumtaka mtuhumiwa huyo katika tarehe ijayo ya kusikiliza kesi hiyo kuja na vithibitisho vya kuaminika bila hivyo sheria itachukua mkondo wake.