Arsene Wenger amejibu mapigo juu ya kauli iliyotolewa na Jose Mourinho aliyoitoa kuhusu kocha huyo wa Arsenal kwamba anatakiwa achukue ‘kalkuleta’ kuhakiki matumizi ya fedha za usajili kwa klabu yake.

Baada ya kauli hiyo kutoka kwa Mourinho, Wenger amekataa kumrushia kijembe Mourinho na kusema kwamba, suala la matumizi ya klabu yake kwa ajili ya usajili liko wazi na namna ambavyo amekuwa akiendeleza wachezaji wake tangu wakiwa na umri mdogo.

Aliwaambia waandishi, “Siku moja mtaona wachezaji ambao tumewaendeleza kutokea hapa halafu mje kufananisha na namna timu nyingine zinavyotumia pesa kwa ajili ya usajili na naamini ninyi wenyewe mtapatwa na mshangao mkubwa sana.”

“Nasikitishwa sana na kauli za watu mbalimbali…mara situmii hela, mara natumia hela sana. Mnawaachia tu watu wazungumze,” alisema.

Wenger pia aliulizwa kuhusu sababu za kushindwa kumsajili Eden Hazard kabla ya Chelsea kumsajili baadaye, akasema kwamba alipungukiwa kiasi kidogo cha fedha ili kuweza kumnasa winga huyo.

Mzee Ojwang kuzikwa leo, Mastaa wa Kenya wajiandaa na Show
Hamad Rashid Aahidi Kujisalimisha Jela