Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ametoa lawama kwa waamuzi kwa kusema viwango vya usimamizi wa mechi katika ligi kuu ya Uingereza vimeendelea kudorora mwaka baada ya mwaka.

Lawama za Wenger zinakuja baada kipigo cha mabao 3-1 ambacho Arsenal walipata jana kutoka kwa Manchester City katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa kwenye uwanja wa Etihad.

Wenger anaamini mshambuliaji wa Man City Raheem Sterling alijiangusha na kupewa penati iliyopigwa na Sergio Aguero dakika ya 50 ambayo iliwasaidia wenyeji kupata bao la pili.

”Nafikiri waamuzi hawafanyi kazi ya kutosha amesema, viwango vinashuka kila msimu kwa sasa na kwa jumla haikubaliki,” alisema Wenger.

City walipata bao la tatu lililofungwa na Gabriel Jesus dakika ya 74 lakini Wenger anaamini bao hilo halikufaa kukubaliwa kwani lilikuwa la kuotea.

Matokeo hayo yameifanya Manchester City kuzidi kujikita kileleni mwa EPL wakiwa na pointi 11 huku Arsenal wakiwa na katika nafasi ya 6 wakiwa na pointi 19 baada ya kucheza michezo 11.

Kigwangalla atumbua jipu kwa kufuatiliwa na watu wasiojulikana
Video: Afande Sele ni Legend lakini hana ufundi wa Hip hop - Wakazi