Meneja wa klabu ya soka ya Arsenal Arsene Wenger ameanza kuangalia mbadala wa nahodha mpya ndani ya kikosi chake kufuatia nahodha wake wa sasa Mikel Arteta kuwa na uwezekano wa kutimka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Mzee Wenger ameanza kumuangalia mlinda mlango wake Petr Cech kuwa Nahodha mpya ndani ya klabu ya soka ya Arsenal.

Wakati kiungo wa Arsenal Mikel Arteta akionekana kutaka kuondoka Emirates Stadium mwezi June mwaka huu , Mzee Arsene Wenger anaangalie mtu wa kuchukua nafasi yake klabu hapo.

Paoja na hayo lakini mlinda mlango namba moja nadani ya klabu hiyo  Cech, anaonekana ana nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo kutokana na kuonekana kuweza kuimudu nafasi hiyo.

Cech’s anaonekana anafasi hiyo kubwa kutokana na kuwa na uwezo wa kuzungumza Lugha 5 kwa wakati mmoja na kuwa na maamuzi mzuri katika kikosi hicho tangu ajiunge nacho akitokea Chelsea.

Alvaro Morata Amfagilia Robert Lewandowski
Mramba,Yona wakabidhiwa kazi za Ofisi