Muungano wa mashirika yanayojihusisha na Saratani nchini – KENCO, unapendekeza watu wenye ugonjwa wa saratani waondolewa ushuru kama inavyofanyika kwa wale walio na ulemavu.
KENCO inapendekeza kuwa, bima ya afya – NHIF, pia igharamie matibabu ya saratani kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Wagonjwa hao walio na saratani pia wanasisitiza uwepo wa wahudumu wa afya wakati wa huduma katika maeneo yao ili kuweza kupata usaidizi wenye tija.