Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kukumbwa na dhoruba la kuwapoteza viongozi wa wake wa ngazi za juu wa mikoa na wilaya wanaotimkia Chadema kumfuata waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Leo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Kahamisi Mgeja na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaa, John Guninita wametangaza kuhamia Chadema.

John Guninita amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa anaona CCM imepoteza muelekeo na sasa inaendeshwa kibabe tofauti na ilivyokuwa mwanzo, huku akitolea mfano uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu ya chama hicho kukata jina la Edward Lowassa katika mchakato wa kura za maoni kumpata mgombea urais, uliohitimishwa kwa kumpata Dk. John Magufuli.

“Watu wanataka mabadiliko, wakiyakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Sasa leo namuenzi baba wa taifa kwa vitendo. Na kutong’ang’ania kwenye chombo ambacho hakitaki mabadiliko, ni kumsaliti baba wa taifa,” alisema Gunitita.

Kwa upande wa Mgeja, alisema kuwa CCM imekosa maadili kwa kuwa hata vijana wadogo wanatumiwa kuwatukana wazee na kisha kupandishwa vyeo.

Jeshi La Polisi Lapiga Marufu Maandamano Ya Wagombea Urais
Mke Wa H Baba Amzuia Kuichezea ‘Toto’