Klabu ya Werder Bremen imepangua hoja za kuzidiwa keta na mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich katika hatua ya kumsajili mshambuliaji wa pembeni Serge Gnabry akitokea Arsenal ya England.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Frank Baumann amesema kuibuliwa kwa hoja za mchezaji huyo kuwa mbioni kusajiliwa na FC Bayern Munich imewasikitisha sana, kutokana na ukweli wa taratibu za mazungumzo yanayoendelea kati yao na The Gunners kufahamika wazi.

Baumann amesema wanatambua hoja zilizoibuliwa jana na baadhi ya vyombo vya habari zina lengo la kuwakatisha tamaa katika mazungumzo yanayoendelea huko jijini London, lakini ameahidi kwamba, hawatochoka kuzungumza na Arsenal na wana uhakika kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo usiku jibu litakua limeshapatikana.

mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, aliesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu ya Arsenal, jana aliripotiwa kuwa katika hatua za mwisho za kujiunga na FC Bayern Munich, baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani iliyoshiriki michuano ya Olimpiki huko nchini Brazil.

Gnabry alijiunga na The Gunners akitokea katika kituo cha kukuza na kuendeleza vijana cha klabu ya Stuttgart mwaka 2011, kwa kipindi alichokaa jijini London alibahatika kucheza michezo 10 ya ligi ya nchini England, kabla ya kupelekwa kwa mkopo West Bromwich Albion msimu uliopita.

Ajitolea kukatwa kichwa kipandikizwe kwa mtu mwingine kwa majaribio
Klabu Kadhaa Zaonyesha Nia Kwa Jack Wilishere