Klabu ya West Ham imerudi tena kwenye mazungumzo na Manchester United ili kuipata huduma ya beki wa kati wa Mashetani Wekundu hao, Harry Maguire kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili juma hili.

Katika mazungumzo hayo mapya, West Ham imetoa ofa ya kutaka kuisaidia Man United kulipa kiasi kidogo cha pesa kwenye kile ambacho wanatakiwa kumlipa Maguire ili aondoke.

Maguire ambaye amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa amedai kutaka kulipwa zaidi ya Pauni 7 milioni ili aondoke.

West Ham ilishafikia makubaliano ya kulipa Pauni 30 milioni na kumsajili Maguire kwa mkataba wa miaka minne kisha kumlipa mshahara wa Pauni 120,000 kwa juma ikiwa ni pungufu ya Pauni 70,000.

Maguire anataka pesa zaidi ama aendelee kusalia Man United ambako anaamini ndani ya miaka miwili iliyobaki atakunja pesa nyingi zaidi ya hiyo ambayo Man United ilitaka kumlipa ili aondoke.

Marufuku vazi la Abaya shuleni yaibua mjadala
Dawa za kulevya zanaswa Iringa, 12 washikiliwa