Muwekezaji mwenza wa klabu ya West Ham Utd, David Gold amethibitisha usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Ghana André Morgan Rami Ayew uliowagharimu kiasi cha Pauni milion 20.

West Ham Utd wamemsaji Ayew akitokea klabu ya Swansea City ambayo aliitumikia msimu uliopita kwa mafanikio makubwa, baada ya kucheza michezo 34 na kufunga mabao 12.

Meneja wa West Ham Utd Slaven Bilic amenukuliwa na vyombo vya habari mara baada ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 “Tunajaribu kuwasajili wachezaji wenye viwango vya hali ya juu, japo katika kikosi changu wapo wenye uwezo wa kupambana.

Ayew ambaye ni mtoto wa gwiji wa soka nchini Ghana Abed Pelle, aliekelea nchini England mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Olympic Marseille.

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yatakiwa kuwachukilia hatua watendaji wote waliohujumu Ushirika
Roberto Mancini Afutwa Kazi Inter Milan