Wagonga nyundo wa London, West Ham Utd, wanaripotiwa kukaribia kumnasa beki wa kati kutoka nchini Italia pamoja na klabu ya Juventus Angelo Obinze Ogbonna.

West Ham Utd ambao wapo chini ya meneja kutoka nchini Croatia, Slaven Bilic watakamilisha usajili wa beki huyo mzaliwa wa nchini Nigeria kwa ada ya uhamisho wa paund milioni 10.

Ogbonna, alijiunga na klabu bingwa nchini Italia, Juventus FC mwaka 2013 akitokea kwa mahasimu wa klabu hiyo nguli katika ligi ya Sirie A, Torino na tayari ameshacheza michezo 31.

Endapo mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, beki huyo mwenye umri wa miaka 27, atakuwa mchezaji wa tano kusajili huko magharibi mwa jijini London.

Waliosajiliwa na klabu ya West Ham Utd mpaka sasa ni Pedro Obiang, Dmitri Payet, Darren Randolph pamoja na Stephen Hendrie.

Wakati huo huo West Ham Utd imefanikiwa kusonge mbele katika michuano ya Europa League, ambayo kwa sasa ipo katika hatua ya mtoano, licha ya kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya FC Lusitans huko nchini Ureno.

Hata hivyo katika mchezo huo mshambuliaji wa kutumainiwa wa klabu ya West Ham Utd, Diafra Sakho alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika 14.

Kardashians Waendelea Kumtonesha Amber Rose Madonda ya Mapenzi
Nape Ayabariki Majina Matano Yaliyopitishwa, Magufuli Asema 'Neno'