Wazee wa kucheza na nyakati na kuwapa watu muziki mzuri, Weusi kutoka Kaskazini wanazisaka saini/sahihi 5000 za mashabiki ‘Waliamshe Dude’.

Wakali hao ambao wimbo wa mwisho ulikuwa ‘Madaraka ya Kulevya’ uliendana na nyakazi ambazo vita dhidi ya dawa za kulevya ilikuwa imeshika kasi kwenye mitandao, wameshapika wimbo waliotohoa kutoka kwenye msemo uliopewa nguvu na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Kupitia mtanda Instagram, Msemaji wa Weusi, Nikki wa Pili amepost kipande cha video kinachowaonesha wakijiachia studio wakicheza wimbo wao huo unaoweza kubatizwa jina la ‘Naliamsha Dude’ na kueleza kuwa akipata maoni 5000 wataiachia ngoma hiyo.

“Tuliamsheee……..nikipata comments elf 5 tuuu……..naliamsha tuu zikitimia,” ameandika Nikki.

Tuliamsheee……..nikipata comments elf 5 tuuu……..naliamsha tuu zikitimia

A post shared by nikk wa ii (@nikkwapili) on


Weusi inaundwa na Nikki wa Pili, Joh Makini, Bonta na G-Nako.

Kibwagizo kinachosikika kwenye wimbo huo huenda kikavuta ‘comments’ zinazotakiwa. Endelea kuwa karibu na Dar24, majibu uatayapata hapa.  

Juma Jux ahitimu masomo, Vanessa awakejeli waliodai picha za darasani
Kamishna Siang'a asema wauza 'Unga' walijaribu kumuua wiki iliyopita