Watumiaji wa mtandao wa ‘Whatsapp’ duniani leo wamekutana na changamoto ya saa kadhaa baada ya mtandao huo kupata matatizo ya kiufundi.
Kwa mujibu wa Independent, watumiaji wengi waliokumbwa na tatizo hilo ni wale waliopo katika maeneo ya Ulaya Magharibi, Pwani ya Mashariki ya Marekani na Marekani ya Kusini. Hata hivyo, imedaiwa kuwa huenda maeneo mengi zaidi duniani yamekumbwa na tatizo hilo ndani ya muda mfupi.
Watumiaji wa mtandao huo katika maeneo yaliyoguswa hawakuwa na uwezo wa kutuma na kupokea jumbe, au hata kufungua jumbe zilizokuwa zimetumwa tayari. Chanzo kinadaiwa kuwa ni matatizo ya ‘server’ zake.
Hii ni mara ya pili kwa mtandao huo pendwa duniani kupata tatizo hilo. Disemba 31, 2015, kwenye mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya mtandao huo ulidaiwa kuzidiwa na kusimama kwa muda.