Kupitia mkutano wa G20 nchini Indonesia. Shirika la Afya Duniani (WHO), limetangaza chanjo tatu za majaribio ya Ebola, ambazo zitawasili nchini Uganda wiki ijayo.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema “Kamati ya wataalam wa nje ya WHO, imetathmini chanjo tatu za wagombea na kukubaliana kwamba wote watatu wajumuishwe katika majaribio yaliyopangwa nchini Uganda.”
Aidha, WHO na Serikali ya Uganda kupitia kwa Waziri wake afya, Jane Aceng wamekubali juu ya mapendekezo ya kamati kwamba dozi ya kwanza ya chanjo itasafirishwa na kuwasili nchini humo kwa muda uliopangwa ili kuanza ktoa huduma hiyo kwa jamii.
Septemba 20, 2022, Waziri huyo wa Afya wa Uganda aliotangaza uwepo wa janga la virusi vya Ebola nchini Uganda, ambalo limesababisha kifo cha mtu mmoja katikati mwa nchi hiyo Wilayani Mubende, ikiwa ni miaka mitatu baada ya kifo cha mwisho kurekodiwa.