Shirika la Afya duniani (WHO), limesema kasi ya janga la virusi vya corona imepungua mnamo juma lililopita, lakini viwango vya vifo vimeongezeka. 

Taarifa hiyo ya WHO imesema kuwa pamoja na kasi kupungua, lakini viwango vya visa vya maambukizi barani Ulaya pamoja na idadi ya vifo bado vipo juu.

WHO imesema kwa juma lililopita Ulaya kuliripotiwa kupungua kwa asilimia 6, kutoka 10 ya wiki nyingine kabla ya hiyo, hatua ambayo masharti ya kujilinda yaliyowekwa katika eneo zima la bara hilo yamesaidia kupunguza kuenea kwa virusi hivyo.

Kwa Afrika shirika hilo lilizingatia maeneo ya ongezeko la maambukizi na vifo katika mataifa ya Afrika Kusini, Algeria na Kenya. 

Hayo yanaarifiwa wakati kukiwa na jumla ya vifo vipya 67,000 vilivyoripotiwa barani Ulaya.

Diego Maradona afariki dunia
Samia kumwakilisha JPM Mkutano wa SADC,Organ Troika