Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeridhia chanjo ya pili ya ugonjwa wa Malaria kwa watoto, ambayo inaweza kuokoa maisha, kwani takriban watoto nusu milioni katika ukanda wa Afrika hufa kila mwaka, kutokana na ugonjwa huo.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amenukuliwa amesema kama mtafiti wa malaria, alikuwa na ndoto kwamba ipo siku ambayo kutakuwa na chanjo salama na yenye ufanisi dhidi ya Malaria.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.Picha ya Esa Alexander/REUTERS.

Amesema, Chanjo mpya ya R21/Matrix-M, iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford cha Uingereza na kuzalishwa na taasisi ya Serum ya India, tayari imeidhinishwa kutumika nchini Burkina Faso, Ghana na Nigeria.

Mwaka 2021, chanjo ya RTS,S iliyotolewa na kampuni kubwa ya dawa ya Uingereza GSK, ilikuwa ya kwanza kupendekezwa na WHO katika kudhibiti ugonjwa wa Malaria kwa watoto, hasa katika maeneo yenye maambukizi ya wastani na juu.

Siku tano za Chongolo, maelekezo ni Umeme
Maandamano: Viongozi wa Upinzani washambuliwa