Shirika la afya duniani – WHO, limetoa tahadhari nyingine juu ya dawa ya kikohozi inayotengenezwa nchini India likisema mchanganyiko wa dawa hiyo ya kunywa unaweza kusababisha madhara au kifo.

Hii inakuwa ni mara ya tano kwa tahadhari hiyo, ambapo miezi 10 iliyopita pia WHO ilitahadharisha juu ya hatari ya dawa hiyo kutoka India, ikisema hali ya maambukizi imekuwa mbaya nchini humo.

Picha ya Milan Berckmans/ AFP.

Kwa mujibu wa WHO, dawa hiyo imebainika kuwa na sumu na kudai kuwa kiwango duni cha dawa hiyo, inayoitwa Cold Out, ni hatari hasa kwa watoto.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni inayotengeneza dawa hiyo, amesema kampuni yake ilitoa tenda kwa kampuni nyingine na kwamba bado haijathibitisha kuokekana sumu katika dawa husika baada ya kuifanyia uchunguzi.

Mapigano yawakimbiza Raia Mil. 3 Sudan, hali bado tete
Fei Toto: Wala wasidhani kama nitapoa