Shirika la Afya ulimwenguni – WHO limearifu kupungua kwa asilimia 90 kwa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Uviko-19, mwongozo wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Monkeypox na kuelezea suala la utapiamlo katika pembe ya Afrika, likisema umefika katika ngazi ya 3 ambayo ni ya juu zaidi.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi hii leo Juni 14, 2023 uliohusu siku ya kimataifa ya uchangiaji wa damu na kuwashukuru wote wanaojitoa kuchangia damu na kuokoa maisha watu.

Amesema, “takwimu zilizopokelewa mpaka sasa nchi 39 zina wagonjwa wa Monkeypox na mpaka sasa tumerekodi jumla ya wagonjwa 1,600 waliothibitishwa na 1500 wanashukiwa kuwa na ugonjwa huo. Kuna vifo 72 katika nchi zilizoathiriwa awali na kwasasa hakuna vifo vipya ila tunafuatilia kuthibitisha taarifa ya kifo huko nchini Brazil kinachohusiana na Monkeypox.”

Kuhusu chanjo ya ndui, Dkt. Tedros amesema inatarajiwa kutoa kinga kidogo dhidi ya Monkeypox, na kwamba kuna takwimu chache za kitabibu na usambazaji wake huku akizitaka nchi zitakazo amua kutumia chanjo hiyo kuzungumza na wananchi watakao patiwa na pia kuhakikisha zinasambazwa kwa usawa kwa wale walio hatarini zaidi kupata mambukizi.

CAF yavuruga akili ya Kocha Mkuu Simba SC
PSG yanawa mikono kwa Kyllan Mbappe