Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa Kundi la mataifa 20 yaliostawi kiuchumi G20 yana uwezo wa kuzuia janga la virusi vya corona kuenea zaidi na kuzuia majanga ya siku zijazo.
Akizungumza wakati wa mazungumzo kuhusu afya kwenye mkutano wa G20 mjini Roma, Ghebreyesus ametoa wito kwa wanasiasa kumaliza mzozo kuhusu chanjo kwa kushughulikia uhaba wa dozi za chanjo hizo kwa mataifa maskini.
Ghebreyesus ameongeza kwamba wanaelewa na kuunga mkono wajibu wa kila serikali wa kulinda raia wake lakini akasema kuwa usawa wa chanjo sio hisani ila ni la manufaa ya kila nchi.
Alitoa wito kwa mataifa hayo ya G20 kusambaza kwa haraka misaada ya chanjo iliyokuwa imeahidiwa na kuunga mkono utengenezaji wa chanjo barani hizo Afrika.